MASOMO YA MISA, APRILI 9, 2017
DOMINIKA YA MATAWI
SOMO 1
Isa. 50:4 – 7
Bwana Mungu amenipa ulimi wa hao
wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka,
huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama
watu wafundishwao. Bwana Mungu amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala
sikurudi nyuma. Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang’oao ndevu mashavu
yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate. Maana Bwana Mungu
atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu
kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 22:7 – 8; 16 – 17a; 18 – 19; 22
– 23 (K)22:1
(K) Mungu wangu, Mungu wangu, mbona
umeniacha?
Wote wanionao hunicheka sana
Hinifyonya, wakitikisa vichwa vyao;
Husema: Umtegemee Bwana; na amponye;
Na amwokoe sasa, maana apendezwa
naye. (K)
Kwa maana mbwa wamenizunguka;
Kusanyiko la waovu wamenisonga;
Yamenizua mikono na miguu.
Naweza kuihesabu mifupa yangu yote.
(K)
Wanagawanya nguo zangu,
Na vazi langu wanalipigia kura.
Nawe, Bwana, usiwe mbali,
Ee Mungu wangu, fanya haraka
kunisaidia. (K)
Nitalihubiri jina lako kwa ndugu
zangu,
Katikati ya kusanyiko nitakusifu.
Ninyi mnaomcha Bwana msifuni
Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo,
mtukuzeni. (K)
SOMO 2
Flp. 2:6 – 11
Ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna
ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana
nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana
mfano wa wanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya
msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo
kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya
duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni
Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
SHANGILIO
Flp. 2:8 – 9
Kristu alijinyenyekeza akawa mtii
hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno,
akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina.
INJILI
Mt. 26: 14 – 27: 66
(Historia ya Mateso ya Bwana)

No comments:
Post a Comment