Siku ya leo ningeomba
tafakati yetu tukiongozwa na kitabu cha Esta wakati wa mfalme Ahausero ambapo Esta
alichaguliwa kua malkia. “Mfaime akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye
akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamria taji ya
kifaime kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti” (Esta 2:17). Katika kipindi hiki cha
ufalme ndipo amri ilitoka kwa mkuu wa maakida aitwae Hamani bin Hamedatha kua
wayahudi wote kuangamizwa (Esta 3:6)
akiwemo Malkia Esta pasipo kujua ni myahudi.
Katika maisha yetu ya
kila siku kabla ya kuumbwa kwetu Mwenyezi Mungu alitujua kabla “Kabla
sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako nalikujua, na kabala hujazaliwa ,
nilikutakasa, na kukuweka uwe nabii wa mataifa” (Yeremia 1:5) Hivyo basi anayajua wazi mambo yanayotunyong’onyesha,
anayajua vyema ambayo yanatukatisha tamaa na kutueka mbali na yeye. “Hamani” apa huenda ikawa ni hali ya ndoa yako, huenda ikawa ni hali
ya kipato chako cha kazi, au huenda
ikawa ni uhusiano wako katika famila
yako,rafiki jamaa na majirani, Hamani anaweza akawa ni matokeo yako shuleni au matokeo duni ya mipanago yako ya kimaisha, afya yako. Mambo ambayo yanatufanya tuwe
mbali na Mwenyez Mungu kwa kutenda dhambi kupitia hayo, kwa namna ya kutegemea
mawazo yetu binafsi na kumsahau yeye muweza wa yote.
Mungu anajua kupanda
kwako na kushuka kwako, anaijua ilipo huzuni yako na anajua ilipo furaha yako
na ndio maana akatupa zawadi pekee ya pendo
lake na kwa hilo ashibisha roho zetu. Ametupatia kibali tangu kuumbwa kwetu kwa
sura na mfano wake kisha kutufanya wafalme tutawale viumbe vyote, ndege wa
angani, samaki wa baharini na wanyama wa porini (Mwanzo 1:26)
Esta kwa kibali
alichopata mbele ya mfalme Ahausero aliweza mshtakia amani juu ya mtesi wake. Alimshtakia
Hamani juu ya adhma yake ya kutaka kuwaangamiza wayahudi wote pamoja na yeye.
aliweza kwa kuongoza na roho wa Mungu kwa sala na toba zilifanywa na wayahudi wote.
(Esta 7:1-6)
Anatulika sote
kusemezana nae, huu ni mualiko muhim kwetu hasa kwa njia ya imani thabiti
iliojengeka mioyo yenu mwetu kwa njia ya kusikia neon lake. Anatualika tumshtaki
‘Hamani’ wetu ni yapi
yanayotuangusha, yapi yanayotukatisha tamaa, yapi yanayotueka mbali na pendo
lake, ni yapo yanataka kutuanagamiza hasa katika sala. Katika sala tunaweza
kushukuru kwa mema mengi Mwenyez Mungu aliotujalia, pia katika sala tunaweza
kumueleza masumbuko yetu. Tuombe
“Nakushukuru
Mungu kwa zawadi ya upendo wako kwengu, na kwa ajili ya mema mengi ulionijalia.
Mbele zako naziweka shida/masumbuko yangu …(zitaje) nikiamin kua wewe ni mwanzo
na mwisho, muweeza wa yote. Nikiomba nguvu mpya na hekima nizidi kupata neema
zako nikitegemea msaada wako nikiyashinda yote kadiri ya mapenzi yako. Nikiomba
hayo yote kwa njia ya Kristu bwana wetu……….”Amina
Novath Ngowi



