Nisomapo sehemu ya Injili ya Luka 7:13 - 14, nafarijika sana na maneno ya Yesu, "..mama usilie". Yesu anajua msiba wangu, matanga yangu, na aibu yangu. Ni Yesu pekee anayejua chozi langu, sononeko langu na kukata tamaa kwangu. Wengine wote wanaonizunguka ni waombolezaji. Yesu anajua nipo ndani ya ndoa yangu kwa miaka kumi, lakini sina hata mtoto wa dawa. Yesu anajua ujane wangu, uyatima wangu. Yesu anajua nipo kitandani nagaagaa kwa maumivu na ugonjwa wa muda mrefu, au ninamuuguza kwa gharama kubwa mwenzangu wa ndoa mgonjwa au mtoto.
Ni Yesu pekee anayejua kazini kwangu kuna majungu na upinzani mkubwa dhidi yangu. Yesu anajua maumivu makubwa niliyonayo kwa vile mwenzangu wa ndoa au mtoto wangu yupo jela. Yesu anajua shida ya mke au mume wangu tuliyetengana kwa muda na uwezekano wa kurudiana ni mdogo. Sauti ya Yesu inaniambia kwa upole katika sikio langu, huku akiwa amegusa bega langu "usilie.."
Ninamuamini Yesu kwa vile ni yeye pekee anajua chozi ni nini. Juu ya msalaba alilia - "eloi eloi lama sabakthani..", alimlilia rafiki yake Lazaro aliyekuwa kaburini kwa siku nne. Na aliulilia mji wa Yerusalemu "Dominus flevit"
Bwana Yesu, kama ulivyomtuliza mjane wa Naini na kumfufua mtoto wake, futa CHOZI langu linalonidondoka asubuhi hii. Futa aibu yangu. Nijalie nisikie tena na tena mwaliko wako, "njoni kwangu ninyi msumbukao na kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.."
Ameeeeen !
Saturday, May 6, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Sefania 3:17 "Yehova Mungu wako yupo katikati yako. Kama Mwenye nguvu, ataokoa.Atakufurahia kwa shangwe. Atanyamaza katika upendo wake...
-
''Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam ni...
-
" Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, 'Usiogope, mimi nitakusaidia" ...
-
Siku ya leo ningeomba tafakati yetu tukiongozwa na kitabu cha Esta wakati wa mfalme Ahausero ambapo Esta alichaguliwa kua malkia. “Mfa...
No comments:
Post a Comment